Monday, June 22, 2015
Msitu mkubwa ulioko kwenye ardhi ya hekari milioni 14 waharibiwa nchini Ivory Coast
na Yusuph Mbogambi
Msitu mkubwa ulioko kwenye ardhi ya hekari milioni 14 waharibiwa nchini Ivory Coast
Waziri wa Maji na Misitu Mathieu Babaud Darret aliarifu kubakia kwa hekari milioni 2 za msitu mkubwa wa hekari milioni 16 kwa uharibifu unaotokana na utafutaji wa ardhi ya kilimo, ujenzi wa makazi na maafa ya moto.
Darret alielezea kwamba ardhi zilizokuwa na msitu zilikuwa ni hekari milioni 9 mwaka wa 1965, na kufikia miloni 3 katika mwaka wa 1991.
Darret pia alisisitiza kwamba serikali imechukuwa hatua thabiti zaidi ikiwa ni pamoja na upandaji wa miti, mbinu bora za kukabiliana na maafa ya moto na kanuni mpya za misitu.
Darret alimalizia kusema kuwa ardhi yenye ukubwa wa hekari 380,000 imeweza kupandwa miti upya kutokana na msaada wa jamii na kanuni mpya ya misitu iliyokubaliwa mwaka 2014.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment