Tuesday, April 21, 2015

KERO UCHAFUZI WA MAZINGIRA MOROGORO

Zimebakia siku chache kuelekea kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ambapo yanafanyika kila June 5 kila mwaka, mwaka jana yalifanyika kitaifa mjini Songea mkoani Ruvuma. Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais mazingira Mh.Dkt. Terezya Huvisa alitoa taarifa kwenye mkutano wa vyombo vya habari kuhusiana na siku hiyo huku akisisitiza uhamasishaji kwa wananchi wote kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhifadhi mazingira. Kaulimbiu ilikua "Panda miti: Hifadhi mazingira" Kaulimbiu hiyo imekuwa tofauti kwa wa kazi wa manispaa Morogoro baada ya kubainika wakitupa takataka ovyo huku wakidai kusubiri gari la manispaa kuziondosha takataka hizo ambapo zinaweza kukaa hadi wiki nzima bila ya kutolewa. Takataka hizo zime kuwa ni hatari kwa binadamu kwasababu zinapo wekwa ni karibu na makazi yao zingine zikiwekwa karibu na milango ya kuingia na kutokea ndani.

Tuesday, April 14, 2015

HISTORIA YA KISIWA CHA CHANGUU ZANZIBAR



HISTORIA YA PRISON ISLAND AU KISIWA CHA CHANGUU. Kisiwa cha changuu ni miongoni mwa kisiwa kidogo kilichomo ndani ya kisiwa cha Zanzibar.kisiwa hicho ni moja ya visiwa vidogo vilivyopo nje kidogo ya bandari ya Zanzibar vilivyopo kisiwa hichi kimebahatika kupata majina tofauti kutokana na shughuli zilizo fanyika ndani yake ``` Miongoni mwa majina ya kisiwa hicho ni changuu,prison island,kibandiko au kisiwa cha Quaratine kisiwa hichi kina urefu wa mita mia nane na upana wamita miatatu.kisiwa hichi kilikuwa hakikaliwi na watu hadi mwaka 1860 wakati sultan wa Zanzibar majid bin said alipo wapa waarabu,ambao walikitumia kisiwa hichi ni jela kwa watumwa watukutu na kuwapeleka nchi nyengine au kuwauza katika soko la watumwala mkunazini mjini Hata hivyo wanunuzi walikuwa wakija na boti ili kuwanunua watumwa hao huko huko na kuwasafirishasehemu mbali mbali kwa mfano wengine walipelekwa india kwa kulima mpunga wapo walio pelekwa oman kwa kulima tende na wengine walibaki hapa hapa Zanzibar kwa kulima karafuu na nazi Mnamo mwaka 1890 zanzibar ilifunga mkataba na ujerumani na ilipelekea kuwekwa miadi na waziri wa uingereza loyal Mathews,kwa kukichukua kisiwa cha changuu na kujengwa jela,na mnamo mwaka 1894 jela ilimalizwa kujengwa. Ila jela haikuwahi kutumika kufungiwa wafungwa hapo ndipo jina la prison island lilipo patikana. Kwa upande wa jina la quaran tine linatokana na marufuku iliyowekwa na serikali ya uingereza kisiwani Zanzibar baada ya kisiwa hicho kugeuzwa hospitali kutokana na maradhi ya kipindu pindu yaliyozuka Zanzibar mwishoni mwaka 1800. Hivyo bandari kubwa ya Afrika Mashariki walibadilisha kisiwa cha changuu na kuwa hospital.na mwaka 1923 kisiwa kilijulikana rasmi kama ni Quarantine island hivyo shughuli zakiQuarantinezilichukuliwa kwa meli na kukaa kati ya wiki moja au mbili kabla kuruhusiwa kuendelea na safari. Meli zilikua zinakuja kutoka December mpaka March hivyo kisiwa kinakua kitupukwa mwaka mzima, wakati kisiwa kinapokuwa kitupu kinakua maarufu kwa sehemu za starehe kwa watu wazungu na wenyeji wa Zanzibar. Nyumba zilizokuwepo ndani ya kisiwa hiki zilijulikana kama ni Bungalow ya wazungu ilijengwa mwaka 1890 kwa ajili ya mapumziko. Hivyon idadi ya watembeaji ilikua kwa kiasi sababu ya maji safi,yalikua mapungufu na yalitegemewa na maji ya mvua ambayo yalihifadhiwa chini ya ardhi kwenye matanki, mapits makubwa yaliyobaki kwenye kisiwa yaliyosafirishwa na kuwa ni bwawa la kuogelea. Majengo ya Quaratine yalijengwa kusini –magharibi mwa kisiwa katika 1931 ambapo yalikuwa na uwezo wa kuchukua watu 904 Vile vile ,kisiwa hiki ni maarufu kwa makobe kobe hao huwa niwakubwa na kufika hadi umri wa miaka 100-200 na kuendelea .kobe hao ni kivutio kikubwa cha watalii wa ndani na nje ya nchi na chakula chao ni majani Asili ya kobe hao wakubwa ,walikuwa ni kobe wa tatu ambao ni zawadi kutoka kwa gavana wa kingereza kutoka kisiwa cha sychelles na badae kuzaliana kwa wingi. Jina la changuu asili yake ni samaki wa changuu ambao wavuvi wali wavua kupitia bahari iliyo zunguka kisiwa hicho . Kwa sasa kisiwa hicho cha prison island na visiwa jirani havina tatizo la maji safi na salama sababu kuna mipira ambayo husambaza maji na kupeleka katika visiwa hivyo. Hata hivyo kivutio kikubwa cha watalii wa ndani na nje katika kisiwa changuu ni magofu ya jela ambayo hayakuwahi kutumika katika shughuli hizo, Makobe wakubwa .Makobe hao hutofautiana muonekano wao kati ya majike na madume ,Madume wamebahatika kuwa na matunungu juu ya magamba yao,wakati jike wapo flati hata hivyo wanaume wapo duara dhidi ya miili yao . hii kwa sababu kipindi cha muingiliano wasiumie sababu ya magamba yao magumu waliyo nayo . Wakati huo inakadiliwa kwa mpaka sasa idadi ya kobe hao wakubwa inaongezeka hadi kufikia 90 mpaka 210 licha ya watu kuwaiba na kwavile kobe ni kiumbe hai huzidi kutaga na idadi kuongezeka kwa kila siku. Kobe pia ana thamani kwa matumizi ya binadam kwani magamba yake hutengenezewa vitu vya mapambo kwa mfano taizi. Pia kwa wenyeji na wageni ambao hutembelea kisiwa hicho hutumia usafiri maalamu wa boti ndogo za mashine ambazo hubeba watu 2 mpaka 11 na malipo yake ni shilingi 30 elfu malipo hayatofautiani kwa wageni na wenyeji hao bali malipo ya kingilio ya kisiwa hicho ni tofauti kwa wenyeji ni shilingi elfu mbili na wageni ni shilingi elfu saba. Hivyo hatuna budi kuvilinda na kuvienzi viumbe hivyo adimu pamoja na mazingira yao kwa ujumla kwani asili haipotei.