Tuesday, April 21, 2015

KERO UCHAFUZI WA MAZINGIRA MOROGORO

Zimebakia siku chache kuelekea kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira duniani ambapo yanafanyika kila June 5 kila mwaka, mwaka jana yalifanyika kitaifa mjini Songea mkoani Ruvuma. Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais mazingira Mh.Dkt. Terezya Huvisa alitoa taarifa kwenye mkutano wa vyombo vya habari kuhusiana na siku hiyo huku akisisitiza uhamasishaji kwa wananchi wote kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhifadhi mazingira. Kaulimbiu ilikua "Panda miti: Hifadhi mazingira" Kaulimbiu hiyo imekuwa tofauti kwa wa kazi wa manispaa Morogoro baada ya kubainika wakitupa takataka ovyo huku wakidai kusubiri gari la manispaa kuziondosha takataka hizo ambapo zinaweza kukaa hadi wiki nzima bila ya kutolewa. Takataka hizo zime kuwa ni hatari kwa binadamu kwasababu zinapo wekwa ni karibu na makazi yao zingine zikiwekwa karibu na milango ya kuingia na kutokea ndani.

No comments:

Post a Comment