Monday, June 22, 2015
Shughuli za uchimbaji madini na uwekaji wa bomba la kusafirishia gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam zimekuwa na mchango mkubwa katika kuathiri mazingira. Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili hivi karibuni unaonyesha kuwa shughuli za uchimbaji madini na nyinginezo zimekuwa zikiathiri watu walioko kwenye maeneo jirani, huku kukiwa hakuna harakati zozote za kuwasaidia wahusika. Kwa mfano mwenyekiti wa Kijiji cha Mahumbika kilichoko Wilaya ya Lindi, Saidi Likandapa anasema misitu ya hifadhi imeharibiwa mno katika mradi wa kupitisha bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam kiasi cha kusababisha baadhi ya vijiji kukosa maji. Anasema kabla ya mradi huo kutekelezwa, tathmini ya athari ya kimazingira haijafanyika na kama ilifanyika haikushirikisha viongozi wa maeneo yaliyopita bomba hilo kama inavyotamka sheria ya usimamizi wa mazingira. Mwenyekiti wa Kijiji cha Madangwa, Wilaya ya Lindi, Abdalah Kidambe anasema kitendo cha viongozi wa vijiji kutoshirikishwa kumechangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira kwani miti mingi imekatwa yakiwamo yale ambayo yalitengwa na vijiji kama maeneo ya hifadhi. Mwenyekiti huyo anasema wizara husika licha ya kutoa fidia kwa wananchi ambao mashamba yao yamechukuliwa kupisha uwekaji wa bomba hilo, pia na vijiji ambavyo bomba hilo limepita navyo vipate fidia kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira uliofanyika. Abrahamu Pasati, mwenyekiti wa wachimbaji wadogo wa Namungo wilayani Ruangwa, Lindi alibainisha kuwa iko haja kwa Serikali kuangalia namna ya kuendesha shughuli hizo kisasa ili zisilete athari. Ameiomba Serikali kuwawezesha wachimbaji hasa wadogo kwa kuwapatia zana za kisasa za kufanyia kazi na kuwajengea uwezo wa namna ya kupunguza uharibifu wa mazingira. Mwenyekiti wa Kijiji cha Chingumbwa wilaya ya Ruangwa, Hamisa Katala ambako machimbo ya Namungo yapo anasema kuwa uharibifu wa mazingira unaofanyika kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini ni mkubwa. “Hivi sasa miti hiyo imeshatoweka na hakuna jihatada ya kurejesha hali yake ya awali, maana yake ni kwamba ukame utaongezeka, wananchi wanaotegemea kilimo watakuwa na hali mbaya zaidi katika siku za baadaye”anasema Hamisa. Anasema wakati umefika kwa Serikali kuangalia kwa umakini mkubwa namna ya kuwasaidia wakazi ili waweze kujenga uhusiano mzuri na wawekezaji. Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Gemen Exploration and Mining Services, Abdalah Kazumba anasema anachofahamu ni kwamba shughuli za uwekezaji wanazofanya hazina athari.
Shughuli za uchimbaji madini na uwekaji wa bomba la kusafirishia gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam zimekuwa na mchango mkubwa katika kuathiri mazingira.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili hivi karibuni unaonyesha kuwa shughuli za uchimbaji madini na nyinginezo zimekuwa zikiathiri watu walioko kwenye maeneo jirani, huku kukiwa hakuna harakati zozote za kuwasaidia wahusika.
Kwa mfano mwenyekiti wa Kijiji cha Mahumbika kilichoko Wilaya ya Lindi, Saidi Likandapa anasema misitu ya hifadhi imeharibiwa mno katika mradi wa kupitisha bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam kiasi cha kusababisha baadhi ya vijiji kukosa maji.
Anasema kabla ya mradi huo kutekelezwa, tathmini ya athari ya kimazingira haijafanyika na kama ilifanyika haikushirikisha viongozi wa maeneo yaliyopita bomba hilo kama inavyotamka sheria ya usimamizi wa mazingira.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Madangwa, Wilaya ya Lindi, Abdalah Kidambe anasema kitendo cha viongozi wa vijiji kutoshirikishwa kumechangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira kwani miti mingi imekatwa yakiwamo yale ambayo yalitengwa na vijiji kama maeneo ya hifadhi.
Mwenyekiti huyo anasema wizara husika licha ya kutoa fidia kwa wananchi ambao mashamba yao yamechukuliwa kupisha uwekaji wa bomba hilo, pia na vijiji ambavyo bomba hilo limepita navyo vipate fidia kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira uliofanyika.
Abrahamu Pasati, mwenyekiti wa wachimbaji wadogo wa Namungo wilayani Ruangwa, Lindi alibainisha kuwa iko haja kwa Serikali kuangalia namna ya kuendesha shughuli hizo kisasa ili zisilete athari.
Ameiomba Serikali kuwawezesha wachimbaji hasa wadogo kwa kuwapatia zana za kisasa za kufanyia kazi na kuwajengea uwezo wa namna ya kupunguza uharibifu wa mazingira.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Chingumbwa wilaya ya Ruangwa, Hamisa Katala ambako machimbo ya Namungo yapo anasema kuwa uharibifu wa mazingira unaofanyika kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini ni mkubwa.
“Hivi sasa miti hiyo imeshatoweka na hakuna jihatada ya kurejesha hali yake ya awali, maana yake ni kwamba ukame utaongezeka, wananchi wanaotegemea kilimo watakuwa na hali mbaya zaidi katika siku za baadaye”anasema Hamisa.
Anasema wakati umefika kwa Serikali kuangalia kwa umakini mkubwa namna ya kuwasaidia wakazi ili waweze kujenga uhusiano mzuri na wawekezaji.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Gemen Exploration and Mining Services, Abdalah Kazumba anasema anachofahamu ni kwamba shughuli za uwekezaji wanazofanya hazina athari.
Msitu mkubwa ulioko kwenye ardhi ya hekari milioni 14 waharibiwa nchini Ivory Coast
na Yusuph Mbogambi
Msitu mkubwa ulioko kwenye ardhi ya hekari milioni 14 waharibiwa nchini Ivory Coast
Waziri wa Maji na Misitu Mathieu Babaud Darret aliarifu kubakia kwa hekari milioni 2 za msitu mkubwa wa hekari milioni 16 kwa uharibifu unaotokana na utafutaji wa ardhi ya kilimo, ujenzi wa makazi na maafa ya moto.
Darret alielezea kwamba ardhi zilizokuwa na msitu zilikuwa ni hekari milioni 9 mwaka wa 1965, na kufikia miloni 3 katika mwaka wa 1991.
Darret pia alisisitiza kwamba serikali imechukuwa hatua thabiti zaidi ikiwa ni pamoja na upandaji wa miti, mbinu bora za kukabiliana na maafa ya moto na kanuni mpya za misitu.
Darret alimalizia kusema kuwa ardhi yenye ukubwa wa hekari 380,000 imeweza kupandwa miti upya kutokana na msaada wa jamii na kanuni mpya ya misitu iliyokubaliwa mwaka 2014.
Subscribe to:
Posts (Atom)